Swali: Ni ipi hukumu ya kukaa pamoja na wasichana wa ami na wasichana wa mjomba na huku Mahram yupo?
Jibu: Ikiwa wamejisitiri na hakuna fitina, basi hapana ubaya. Ama ikiwa kukaa huko ni kwa ajili ya fitina au kwa ajili ya kufurahia kuwaangalia wakiwa hawakujisitiri, basi hilo halijuzu. Lakini kukaa nao kwa ajili ya kuwasalimia au kuuliza hali ya mgonjwa wao na huku wakiwa wamejisitiri na wamevaa Hijaab na wakiwa mbali na fitina kwa njia ya heshima na adabu, basi hapana neno. Hivi ndivyo waislamu wanavyopaswa kuwa baina yao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3184/حكم-الجلوس-مع-بنات-العم-او-الخال
- Imechapishwa: 30/07/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kukaa pamoja na wasichana wa ami na wasichana wa mjomba na huku Mahram yupo?
Jibu: Ikiwa wamejisitiri na hakuna fitina, basi hapana ubaya. Ama ikiwa kukaa huko ni kwa ajili ya fitina au kwa ajili ya kufurahia kuwaangalia wakiwa hawakujisitiri, basi hilo halijuzu. Lakini kukaa nao kwa ajili ya kuwasalimia au kuuliza hali ya mgonjwa wao na huku wakiwa wamejisitiri na wamevaa Hijaab na wakiwa mbali na fitina kwa njia ya heshima na adabu, basi hapana neno. Hivi ndivyo waislamu wanavyopaswa kuwa baina yao.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3184/حكم-الجلوس-مع-بنات-العم-او-الخال
Imechapishwa: 30/07/2026
https://firqatunnajia.com/mtu-kukaa-pamoja-na-mabinamu-zake-na-watoto-wa-mjomba/