Benki imempa faida ya pesa zake alizozihifadhi kwa muda mrefu

Swali: Niliweka fedha zangu katika benki muda mrefu uliopita na nilipokuja kuzichukua wakaniambia kwamba hizi ni faida zako takriban 50,000 SAR. Nimejua kuwa hii ni ribaa na si halali kwangu. Sasa nauliza: katika kijiji chetu kuna kisima ambacho ni chanzo cha maji kwa kijiji ambacho watu wanakunywa humo. Je, inafaa niweke fedha hizi katika kukipanua na kuongeza maji ili watu wanufaike zaidi?

Jibu: Ndiyo. Ikiwa mtu amechukua mali kama hii au imeingia kwake mali isiyo halali kwa mujibu wa Shari´ah, basi anapaswa kuitoa katika maslahi ya waislamu na katika njia za kheri. Mfano wake ni mali iliyoporwa ambayo mwenyewe hajulikani au amesahaulika, basi hutolewa swadaqah kwa masikini au huwekwa katika maslahi ya waislamu. Hivyo kuipanua kisima, kukijengea uzio na kuboresha huduma yake ni katika maslahi ya waislamu. Vivyo hivyo anaweza kuitumia kuwalisha masikini, kulipa madeni ya wadaiwa au kusaidia ndoa za wenye uhitaji. Mambo yote haya ni katika maslahi ya waislamu na hairuhusiwi yeye kuitumia kwa nafsi yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3177/صرف-المال-الربوي-في-مصالح-المسلمين
  • Imechapishwa: 30/07/2026