Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kufunua uso wake mbele ya afisa wa ukaguzi wa pasipoti?

Jibu: Ikiwa kuna dharurah ya kusafiri, basi anaweza kusamehewa katika hilo. Ama ikiwa si dharurah, basi hafunui uso wake, bali arejee na aache kusafiri. Lakini ikiwa ni dharurah ya kusafiri na haiwezekani kusafiri isipokuwa kwa kupigwa picha au kufunua uso wake, basi haionekani kuwa na kizuizi katika hali ya dharurah hiyo. Ama ikiwa safari si ya lazima, basi asisafiri na asifunue uso wake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3174/حكم-كشف-المراة-وجهها-عند-ضابط-امن-المطار
  • Imechapishwa: 30/07/2026