Swali: Wakati wa ndoa baadhi ya watu hutoka na kuchinja mbele ya bwanaharusi na bibiharusi na kunyunyizia chumvi. Unasemaje juu ya hilo?
Jibu: Ni ukhurafi. Ikiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amekadiria wanaharusi kuishi kwa furaha, basi watafanya hivo:
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
“Miongoni mwa alama Zake ni kwamba amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao na amekujaalieni kati yenu mapenzi na huruma. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanaotafakari.”[1]
Ikiwa Allaah hakulitaka hilo basi haijalishi kitu chochote unachofanya. Pengine wakamwacha bibiharusi nje ya mlango mpaka ijitokeze nyota fulani. Wakati mwingine wanabaki wamesimama nje katika hali ya hewa yenye baridi na wanapatwa na mafua na wanasubiri mpaka ijitokeze nyota fulani. Wanajimu wana mambo ya ukhurafi na ya upuuzi. Ikiwa mwanamke anaitwa Zaynab wanamwambia kuwa jina lake haliendani na jina la mume na hivyo wanamwamrisha kubadilisha jina lake kwenda Swaalihah, Faatwimah au ´Aaishah.
[1] 30:21
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 29-30
- Imechapishwa: 29/01/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)