Wakati Ahl-us-Sunnah wanaposema kuwa jambo fulani ni shirki, kufuru, dhuluma au dhambi, basi hawasema hivo isipokuwa ni kutokana na dalili. Wakati Ahl-us-Sunnah wanaposema kuwa kumwomba mwingine asiyekuwa Allaah ni shirki, basi Qur-aan na Sunnah vinashuhudia jambo hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚإِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ
“Yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wowote juu ya hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake, kwani hakika hawafaulu makafiri.”[1]
Allaah amemwita kuwa ni “kafiri”. at-Tirmidhiy amepokea kupitia kwa an-Nu´maan bin Bashiyr ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Du´aa ni ´ibaadah.”
Kisha akasoma maneno Yake (Ta´ala):
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚإِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ
“Mola wenu amesema: “Niombeni Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na ‘ibaadah Yangu, wataingika Motoni wadhalilike.””[2]
Vivyo hivyo juu ya shirki. Ahl-us-Sunnah wanalazimiana na dalili. Isitoshe wanapambanua kati ya shirki kubwa na shirki ndogo, kufuru kubwa na kufuru ndogo, unafiki mkubwa wa kiimani na unafiki mdogo wa kimatendo.
[1] 23:117
[2] 40:60
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 33-34kufu
- Imechapishwa: 29/01/2025
Wakati Ahl-us-Sunnah wanaposema kuwa jambo fulani ni shirki, kufuru, dhuluma au dhambi, basi hawasema hivo isipokuwa ni kutokana na dalili. Wakati Ahl-us-Sunnah wanaposema kuwa kumwomba mwingine asiyekuwa Allaah ni shirki, basi Qur-aan na Sunnah vinashuhudia jambo hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚإِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ
“Yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wowote juu ya hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake, kwani hakika hawafaulu makafiri.”[1]
Allaah amemwita kuwa ni “kafiri”. at-Tirmidhiy amepokea kupitia kwa an-Nu´maan bin Bashiyr ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Du´aa ni ´ibaadah.”
Kisha akasoma maneno Yake (Ta´ala):
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚإِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ
“Mola wenu amesema: “Niombeni Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari na ‘ibaadah Yangu, wataingika Motoni wadhalilike.””[2]
Vivyo hivyo juu ya shirki. Ahl-us-Sunnah wanalazimiana na dalili. Isitoshe wanapambanua kati ya shirki kubwa na shirki ndogo, kufuru kubwa na kufuru ndogo, unafiki mkubwa wa kiimani na unafiki mdogo wa kimatendo.
[1] 23:117
[2] 40:60
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 33-34kufu
Imechapishwa: 29/01/2025
https://firqatunnajia.com/pindi-ahl-us-sunnah-wanaposema-jambo/