Swali: Kaka yangu ameoa na ana watoto wane. Haswali. Je, una maneno mazuri au nasaha ya kumpa?

Jibu: Haswali? Haswali na Jamaa´ah? Ikiwa haswali na Jamaa´ah ameacha jambo la wajibu na ni dhambi. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah. Swalah yake ni sahihi. Hata hivyo Hadiyth inasema Swalah kwa Jamaa´ah ni bora mara ishirini na saba kuliko kuswali peke yake.

Ama ikiwa haswali kabisa, Uislamu sio Dini yake. Ni kafiri. Mwenye kuacha Swalah kwa kukusudia mpaka wakati wake ukatoka ni kafiri. Ni juu yake kutubu kwa Allaah na kuhifadhi Swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqu-%2020-08-1435.mp3
  • Imechapishwa: 09/04/2015