Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

126 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameelezakuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

 بَينَما رَجُلٌ يَمشي بِطَريقٍ اشْتَدَّ عَلَيهِ العَطَشُ، فَوَجَدَ بِئرًا فَنَزَلَ فِيهَا فَشربَ، ثُمَّ خَرَجَ فإذَا كَلْبٌ يَلْهَثُ يأكُلُ الثَّرَى مِنَ العَطَشِ، فَقَالَ الرَّجُلُ: لَقَدْ بَلَغَ هَذَا الكَلْبُ مِنَ العَطَشِ مِثلُ الَّذِي كَانَ قَدْ بَلَغَ مِنِّي فَنَزَلَ البِئْرَ فَمَلأَ خُفَّهُ مَاءً ثُمَّ أمْسَكَهُ بفيهِ حَتَّى رَقِيَ، فَسَقَى الكَلْبَ، فَشَكَرَ الله لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ. قالوا: يَا رَسُول اللهِ، إنَّ لَنَا في البَهَائِمِ أَجْرًا؟ فقَالَ: في كُلِّ كَبِدٍ رَطْبَةٍ أجْرٌ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

وفي رواية للبخاري: فَشَكَرَ اللهُ لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ، فأدْخَلَهُ الجَنَّةَ

وفي رواية لهما: بَيْنَما كَلْبٌ يُطِيفُ بِرَكِيَّةٍ قَدْ كَادَ يقتلُهُ العَطَشُ إِذْ رَأَتْهُ بَغِيٌّ مِنْ بَغَايَا بَنِي إسْرَائِيل، فَنَزَعَتْ مُوقَها فَاسْتَقَتْ لَهُ بِهِ فَسَقَتْهُ فَغُفِرَ لَهَا بِهِ

“Kulikuwa na mtu aliyekuwa akitembea na ghafla akashikwa na kiu ambapo akaona kisima na akawa ameteremka na kunywa maji. Alipokuwa anatoka kwenye kisima kile akaona mbwa yuwahema na huku anakula udongo kutokana na kiu. Yule mtu akasema mbwa huyu ameshikwa na kiu kama nilichokuwa nacho. Akateremka kwenye kisima na kujaza soksi yake maji na huku ameyazuia na mdomo wake na kwenda kwa yule mbwa na akamnywesha. Yule mbwa akamshukuru na hiyo ndio ikawa sababu ya Allaah kumsamehe.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Kwani sisi tuna ujira kwa wanyama?” Akasema: “Kuna ujira kwa kunywesha kila kilicho hai.”[1]

Katika upokezi mwingine, na huenda ni kisa kingine, kuna mwanamke malaya katika wanawake wa wana wa israaiyl aliona mbwa aliyekuwa na kiu. Lakini hata hivyombwa huyo hawezi kuyafikia maji kwa kuwa yalikuwa kwenye kisima. Mwanamke huyo akawa ameteremka yeye kwenye kisima hicho na kumnywesha huyo mbwa. Hiyo ikawa ni sababu ya Allaah kumsamehe. Hii ni dalili inayoonyesha kuwa wanyama wana ujira.

Mnyama yoyote unayemtendea wema kwa kumnywesha, kumlisha, kumlinda na jua kali au baridi kali – haijalishi kitu ni mamoja ikiwa ni mnyama wako au mnyama wa mtu mwingine au anayemilikiwa na watu wengi – una ujira kwa hilo mbele ya Allaah (´Azza wa Jall). Hawa ni wanyama! Tusemeje juu ya wanadamu? Ukiwatendea wema wanadamu inakuwa bora zaidi na ujira mkubwa.

[1] al-Bukhaariy na Muslim

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/173)
  • Imechapishwa: 03/06/2024