Swali: Je, asili ya imani kwa waumini wote ni sawa au inatofautiana kati ya mtu na mtu?
Jibu: Asili ya imani ni moja, nayo ni kumuamini Allaah, Mitume Wake, Malaika Wake, Vitabu Vyake, siku ya Mwisho na kila alilolieleza Allaah na Mtume Wake. Lakini imani hutofautiana; si imani ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na Maswahabah wengine kama imani ya waliokuja baada yao. Inatofautiana katika nguvu, ukamilifu, utimilifu na athari yake. Lakini asili yake ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mtume Wake, siku ya Mwisho, makadirio ya kheri yake na shari yake, kuamini kila alichokifanya kuwa Shari´ah Allaah na Mtume Wake, kuamini kila alichokieleza Allaah na Mtume Wake kuhusu mambo ya Aakhirah, Pepo na Moto na mengineyo. Lakini imani hii huongezeka na kuwa na nguvu kwa elimu, juhudi, kufahamu dini, wivu kwa ajili ya Allaah na kumcha Allaah mpaka mja anatekeleza wajibu na kuacha yaliyoharamishwa. Kama ambavyo imani hii hupungua kwa ujinga, kupuuza, kukaa na waovu na kufuata matamanio.
Kwa hiyo wanazuoni wamesema kuwa imani huongezeka na hupungua; huongezeka kwa utiifu na hupungua kwa maasi. Hivyo imani ni maneno kwa ulimi, matendo kwa viungo na matendo ya moyo pamoja na kuamini kwake. Mwenye kufanikiwa kupewa elimu yenye manufaa, uoni sahihi, kumcha Allaah, kukaa na watu wema na kufuata mwenendo wa watu wema, basi imani yake huongezeka, kuinuka na kukamilika. Mwenye kuwa kinyume na hilo kwa ujinga wake, kufuata matamanio yake au kukaa na waovu, haya ni miongoni mwa sababu za kudhoofisha imani. Inaweza kudhoofika sana mpaka ikaondoka kabisa na ikamtoa mtu katika dini, au kudhoofika chini ya hapo kwa sababu ya maasi. Ndiyo maana wanazuoni wamesema: huongezeka kwa utiifu na hupungua kwa maasi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3366/حقيقة-اصل-الايمان-وتفاوت-الناس-فيه
- Imechapishwa: 20/08/2026
Swali: Je, asili ya imani kwa waumini wote ni sawa au inatofautiana kati ya mtu na mtu?
Jibu: Asili ya imani ni moja, nayo ni kumuamini Allaah, Mitume Wake, Malaika Wake, Vitabu Vyake, siku ya Mwisho na kila alilolieleza Allaah na Mtume Wake. Lakini imani hutofautiana; si imani ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na Maswahabah wengine kama imani ya waliokuja baada yao. Inatofautiana katika nguvu, ukamilifu, utimilifu na athari yake. Lakini asili yake ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mtume Wake, siku ya Mwisho, makadirio ya kheri yake na shari yake, kuamini kila alichokifanya kuwa Shari´ah Allaah na Mtume Wake, kuamini kila alichokieleza Allaah na Mtume Wake kuhusu mambo ya Aakhirah, Pepo na Moto na mengineyo. Lakini imani hii huongezeka na kuwa na nguvu kwa elimu, juhudi, kufahamu dini, wivu kwa ajili ya Allaah na kumcha Allaah mpaka mja anatekeleza wajibu na kuacha yaliyoharamishwa. Kama ambavyo imani hii hupungua kwa ujinga, kupuuza, kukaa na waovu na kufuata matamanio.
Kwa hiyo wanazuoni wamesema kuwa imani huongezeka na hupungua; huongezeka kwa utiifu na hupungua kwa maasi. Hivyo imani ni maneno kwa ulimi, matendo kwa viungo na matendo ya moyo pamoja na kuamini kwake. Mwenye kufanikiwa kupewa elimu yenye manufaa, uoni sahihi, kumcha Allaah, kukaa na watu wema na kufuata mwenendo wa watu wema, basi imani yake huongezeka, kuinuka na kukamilika. Mwenye kuwa kinyume na hilo kwa ujinga wake, kufuata matamanio yake au kukaa na waovu, haya ni miongoni mwa sababu za kudhoofisha imani. Inaweza kudhoofika sana mpaka ikaondoka kabisa na ikamtoa mtu katika dini, au kudhoofika chini ya hapo kwa sababu ya maasi. Ndiyo maana wanazuoni wamesema: huongezeka kwa utiifu na hupungua kwa maasi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3366/حقيقة-اصل-الايمان-وتفاوت-الناس-فيه
Imechapishwa: 20/08/2026
https://firqatunnajia.com/uhakika-wa-asili-ya-imani-unatofautiana-kwa-watu/