Swali: Je, Hijaab iliteremshwa mahsusi kwa wanawake huru waislamu tu na haikulazimishwa kwa wajakazi, ilhali wajakazi nao wana kishawishi hichohicho? Je, ni sahihi kwamba ´Umar bin al-Khatwaab (Radhiya Allaahu ´anh) alimkataza mmoja wa wajakazi kuvaa Hijaab na kujifananisha na wanawake waungwana?

Jibu: Asili ni kwamba Hijaab ni kwa wanawake huru. Hii ndiyo asili. Wajakazi wako katika kazi za huduma na mara nyingi wao si wenye khatari kwa upande wa kujisitiri waziwazi, kwa upande wa uzuri. Wanawake huru wanawajibika kujisitiri na kuvaa Hijaab. Wanazuoni wengi (Rahimahu Allaah) wametaja kwamba mjakazi ikiwa ana uzuri na ana mvuto, pia anawajibika kujisitiri. Kwa sababu sababu ni ileile. Ikiwa hana uzuri, anakuwa kama mwanamke mzee, halazimiki kuvaa Hijaab. Mwanamke mzee mkubwa ambaye hataki kuolewa na wala hajipambi, naye ni katika wale wazee waliokaa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَالْقَوَاعِدُ مِنَ النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَاتٍ بِزِينَةٍ

”Wanawake wazee waliokatika hedhi ambao hawataraji kuolewa, hakuna ubaya juu yao kupunguza baadhi ya nguo zao bila ya kudhihirisha mapambo yao.”[1]

Mwanamke mzee ambaye hatamaniwi, hajipambi wala hafanyi yanayovutia kuolewa na mjakazi ambaye hakuna khatari juu yake, hawala ulazima wa Hijaab.

[1] 24:60

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3371/حكم-اختصاص-الحجاب-بالحراىر-من-المسلمات-دون-الاماء
  • Imechapishwa: 20/08/2026