Hapana neno kumuomba ndugu yako akuombee du´aa

Swali: Je, inajuzu kwa mtu kumuomba mtu mwema amuombee du´aa? Ikiwa inajuzu, basi mimi ninaomba kutoka kwenu na waliopo hapa mniombee du´aa kwamba Allaah anirahisishie kuhifadhi Qur-aan, anipe ufahamu katika dini, aniruzuku uwezo wa kufasiri, anifanye niwe na manufaa kwa waislamu, pamoja na wema na kumtakasia nia Allaah katika maneno na matendo, itikieni ”Aamiyn”?

Jibu: Aamiyn, Allaah akurekebishe, akurahisishie mambo yako, akuruzuku kuhifadhi Qur-aan Tukufu, kuitendea kazi na anihidi mimi na wewe na waislamu wote katika njia Yake iliyonyooka. Hakuna ubaya. Inajuzu kwa muislamu kumwambia ndugu yake: niombee kwa Allaah, ee ndugu yangu, niombee kwa Allaah aniongoze, niombee Allaah anisamehe. Hakuna ubaya. Hili halina tatizo, lakini hawaombwi waliokufa. Wenye kuombwa ni walio hai tu. Anamwambia aliye hai: ee ndugu yangu niombee kwa Allaah kwamba anisamehe, niombee kwa Allaah anirahisishie mke mwema na watoto wema. Hakuna ubaya. Ama kwenda kwa waliokufa na kuwaomba walio mbali ”Ee bwana wangu al-Badawiy”, ”Ee bwana wangu al-Husayn”, ”Ee fulani nisaidie na uniombee”, hili ni jambo ovu. Hili halifai. Hii ni katika shirki kubwa. Tunamuomba Allaah atulinde.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3369/حكم-طلب-الدعاء-من-الصالحين
  • Imechapishwa: 20/08/2026