Ameongeza mke kabla ya eda ya aliyemwacha kumalizika

Swali:  Vipi ikiwa mwanaume ana wake wanne, kisha akamtaliki mmoja wao na akaoa mwingine kabla ya kumalizika kwa eda ya yule aliyetalikiwa?

Jibu: Hana ruhusa ya kufanya hivyo. Haijuzu kwake kuoa mpaka atoke kwenye eda. Ikiwa ni talaka rejea, haijuzu kwake kwa maafikiano ya waislamu. Kwa sababu bado ni mke. Yule wa kurejea ikiwa amemtaliki talaka moja au mbili, basi ni wa kurejea. Katika hali hiyo hana ruhusa ya kuoa wa tano mpaka huyu atoke kwenye eda.

Ikiwa talaka ni ya mwisho isiyokuwa ya kurejea, basi kuna maoni tofauti baina ya wanazuoni. Kinachotakikana ni kwamba asioe. Haya ndio maoni sahihi; kwamba asifunge ndoa mpaka atoke ndani ya eda kwa ajili ya kufunga kufunga mlango wa kulegeza mambo na kuzuia njia ya kuoa katika eda nyingine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3388/حكم-الزواج-بالخامسة-قبل-تمام-عدة-الطلاق-للرابعة
  • Imechapishwa: 20/08/2026