Swali: Je, kumethibiti dalili juu ya kuharamishwa kuswali kwenye misikiti ilio na makaburi au hili ni kwa njia tu ya kuziba njia [zinazopelekea katika shirki]?

Jibu: Ametakasika Allaah! Hakukuthibiti dalili? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tanabahini! Msiyafanye makaburi kuwa misikiti.”

Bi maana msiswali kwenye makaburi. Neno “Msikiti” haina maana tu ya jengo, bali maana yake ni kuswali kwenye makaburi. Yule mwenye kuswali mahali fulani amepafanya mahali hapo kuwa Msikiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ardhi yote imefanywa kwangu kuwa Msikiti na safi.”

Kuswali kwenye makaburi ni kuyafanya kuwa misikiti hata kama kutakuwa hakuna misikiti uliojengwa. Haijuzu kufanya hivi. Mtume amekataza hili katika Hadiyth nyingi. Ameeleza kuwa ni katika matendo ya mayahudi na manaswara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (48) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-5-26.mp3
  • Imechapishwa: 27/08/2020