Uelewa wa kimakosa wa baadhi ya watu kutoulizia wanayoyahitajia

Katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si sawa kuulizia juu ya kitu kilichonyamaziwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Niacheni kwa yale niliyokuachieni. Hakika kilichofanya kuangamia waliokuwa kabla yenu ni kuuliza kwao kwa wingi na kupingana na Mitume wao.”[1]

Ama leo na baada ya Wahyi kukatika kwa kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uliza. Uliza juu ya kila kitu unachokihitajia kwa kuwa mambo yametulia leo; hakuna kitachozishwa wala kupunguzwa. Ama wakati Wahyi bado unateremshwa kuna uwezekano kukazidishwa au kupunguzwa kitu. Baadhi ya ´Awwaam wanafahamu kuhusiana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ

“Enyi mlioamini! Msiulizie mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.” (05:101)

Vilevile kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Niacheni kwa yale niliyokuachieni.”

wanafahamu uelewa wa kimakosa. Utawaona wanafanya mambo ya haramu na wanaacha mambo ya wajibu na haulizi. Hali imefikia kwamba kuna ambao wanaambiwa “Jambo hili ni haramu, wawaulize wanachuoni” wanajibu kwa kusema:

لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ

“Msiulizie mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.”

Hili halijuzu. Lililo la wajibu kwa mtu ni ajifunze dini ya Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri, basi humpa ufahamu akaielewa dini.”[2]

[1]al-Bukhaariy (7688) na Muslim (1337).

[2]al-Bukhaariy (81) na Muslim (1037).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/271-272)
  • Imechapishwa: 29/10/2024