Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

74 – Aliyajua pia matendo yao watakayofanya.

75 – Kila mmoja amewepesishiwa kwa kile alichoumbiwa.

MAELEZO

Aliyajua matendo yao kwa utambuzi Wake wa milele.

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kila mmoja amewepesishiwa kwa kile alichoumbiwa.”

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ

“Basi yule anayetoa na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza na akakadhibisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.”[1]

[1] 92:5-10

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 30/10/2024