Tumezungumzia kuhusu uchaguzi na kusema kuwa ni Twaaghuut na kwamba bunge ni Twaaghuut. Tumezungumzia mambo yanayoenda kinyume na dini ya Allaah. Tumeyaraddi kwenye vitabu “al-Muswara´ah”, “Qam´-ul-Mu´aanid”, “Ghaarat-ul-Ashritwah” na vingine.

Watu wanajua msimamo wetu kwa chaguzi hizi za ki-Twaaghuut na bunge hizi za ki-Twaaghuut. Lakini haina maana wale wenye kukaa bungeni ni makafiri. Hata hivyo wana sehemu ya Twaaghuut kivyake kutegemea na mapenzi ya mtu kwa bunge.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Burkaan, uk. 22
  • Imechapishwa: 26/08/2020