Kuna mtu amesema:

“Mwenye kumtii mtawala ambaye anaamrisha kanuni za kibinaadamu katika suala limoja, anatoka katika Uislamu.”[1]

Kwa njia hiyo, anasema yeye mwenyewe ya kwamba ni kafiri. Kwa kuwa amewatii wengi wasiokuwa Allaah katika mambo mengi na si katika suala moja tu. Mtu huyu ananyoa ndevu zake. Alikuwa anamtii nani sasa? Je, alikuwa anamtii Allaah wakati anaponyoa ndevu zake? Mtu huyu alikuwa na anavaa tai. Je, alikuwa anamtii Allaah sasa? Alikuwa na makosa mengi ya kifikra na kiitikadi. Alikuwa anamtii nani sasa? Mtu huyu ni masikini. Anajikufurisha yeye mwenyewe bila ya kujua hilo. Madhehebu haya ni khatari sana.

[1] Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan (3/1198).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/111-112)
  • Imechapishwa: 26/08/2020