Swali: Kuna kigezo kipi cha kufanya uadilifu katika kulala kwa mwanaume ambaye ana wake wengi? Je, inamlazimu kulala naye katika chumba kimoja au inatosha endapo atalala chumba kingine nyumbani kwake?
Jibu: Kinachotakikana ni yeye kulala nyumbani kwake. Si lazima kulala naye katika kitanda kimoja.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (38)
- Imechapishwa: 22/06/2023