Allaah (Ta´ala) amesema:

طه مَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لِتَشْقَىٰ

“Twaa Haa. Hatukukuteremshia Qur-aan ili upate mashaka.”[1]

“Twaa” na “Haa” ni herufi mbili za mkato. Sio jina miongoni mwa majina ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama walivodai baadhi ya watu. Ni herufi za mkato ambazo Allaah ameanza nazo katika baadhi ya Suurah Tukufu katika Qur-aan. Ni herufi zisizokuwa na maana. Kwa kuwa Qur-aan imeteremka kwa lugha ya kiarabu. Lugha ya kiarabu haifanyi herufi za mkato zikawa na maana. Isipokuwa mpaka pale zinapoambatanishwa na kufanya ikawa neno.

[1] 20:01-02

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/210)
  • Imechapishwa: 10/09/2024