Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

142 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa:

أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم دخل عَلَيْهَا وعِندها امرأةٌ، قَالَ: (مَنْ هذِهِ؟) قَالَتْ: هذِهِ فُلاَنَةٌ تَذْكُرُ مِنْ صَلاتِهَا. قَالَ: (مهْ، عَلَيْكُمْ بِمَا تُطِيقُونَ، فَواللهِ لا يَمَلُّ اللهُ حَتَّى تَمَلُّوا، وكَانَ أَحَبُّ الدِّينِ إِلَيْهِ مَا دَاوَمَ صَاحِبُهُ عَلَيهِ) مُتَّفَقٌ عَلَيه

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwake na yuko pamoja na mwanamke [mwenzake]. Akamuuliza: “Nani huyu?” Akamwambia: “Huyu ni fulani. Akataja kuhusu swalah zake [anavoswali sana].” Akamwambia: “Koma!” Fanyeni mnachoweza. Ninaapa kwa Allaah kuwa Allaah hachoki mpaka nyinyi mchoke. Kinachopendeza zaidi Kwake ni kile ambacho mwenye nacho anadumu juu yake.”[1]

Maana ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha mwanamke huyu akome na kufanya matendo mengi ambayo yanaweza kuja kumkuia mazito. Matendo ambayo yanaweza kumkuia magumu na akashindwa huko mbele na hivyo asidumu kwayo. Kisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha tufanye matendo kwa kiasi na tunavyoweza:

“Fanyeni mnachoweza.”

Bi maana msizikalifishe nafsi zenu. Mtu akiikalifisha nafsi yake na kupambana nayo huchoka na kupunguza na halafu hatimaye anaacha.

[1] al-Bukhaariy na Muslim

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/212-213)
  • Imechapishwa: 10/09/2024