Tususie chakula cha mtu anayekula ribaa?

Swali: Inajuzu kumtenga mtu anayefanya biashara ya ribaa na kutokula chakula anachotuletea?

Jibu: Anatakiwa kunasihiwa, kumkumbusha juu ya Allaah (´Azza wa Jall), kumletea Aayah na Hadiyth ambazo ndani yake kuna matahadharisho juu ya ribaa na maneno ya wanachuoni. Huenda akatubia kwa Allaah (´Azza wa Jall).

Kuhusu kula chakula chake, ikiwa hana chumo lingine zaidi ya hii ribaa haifai kula chakula chake kwa sababu ni cha haramu. Ama ikiwa ikiwa yuko na mali iliyochanganyikana na halali na haramu, hakuna neno kula chakula chake kwa sababu mtu hawezi kuyakinisha kuwa kimetokamana na ribaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaath-il-Usuwl (05) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/charh-el-osol-el-thalatha/charh-fwzan/05.mp3
  • Imechapishwa: 18/01/2019