Tusi kwa tusi, kusamehe bora zaidi

Swali: Mtu anapokutukana kwa maneno haramu inafaa kumjibu kwa mfano wake?

Jibu: Ndiyo, kwa mujibu wa maneno Yake:

فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ

Basi atakayekufanyieni uadui, basi nanyi mfanyieni uadui kwa kadiri alivyokufanyieni uadui.” (02:194)

Kwa hiyo akikwambia: ”Allaah akulaani!” nawe mjibu kwa kusema ”Nawe Allaah akulaani!”. Hata hivyo kusamehe na kuacha kujibu ni bora zaidi, kama alivosema Allaah:

وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ

”Mkilipiza kisasi, basi lipizeni kisasi kulingana na vile mlivyoadhibiwa; na mkifanya subira, basi hapana shaka hivyo ni bora zaidi kwa wenye kufanya subira.” (16:126)

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25217/هل-يجوز-الرد-بالمثل-على-من-سب-بلفظ-محرم
  • Imechapishwa: 18/02/2025