Tunaambiwa “Wahhaabiyyah” tunapokataza shirki

Swali: Leo tunaona waabudu makaburi wengi al-Madiynah al-Munawwarah wanadhihirisha shirki zao mbele ya umati na wanajipangusa kwa bwana na kwenye kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tunapowanasihi wanatucheza shere na kutwambia “nyinyi ni Wahhaabiyyuun”. Tuwafanye nini?

Jibu: Lililo la wajibu kwenu ni kuwakemea kwa ulimi kwa njia ya kuwabainishia. Wasipopokea nasaha pelekeni suala lao kwa kwenda kuwashtaki kwa wasimamizi [sauti haiko wazi] wa al-Madiynah, kamati [ya wanachuoni wakubwa] au Maktabah ya Da´wah. Wafikishieni wasimamizi. Hili ndio la wajibu kwenu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2104
  • Imechapishwa: 28/06/2020