Swali: Je, inajuzu kunyoa pande za mashavu? Ni ipi hukumu ya kupunguza ndevu? Je, kupunguza ndevu ni sawa na kunyoa?
Jibu: Ndevu ni heshima aliyopewa mwanaume na Allaah. Allaah ameifanya kuwa ni sifa ya pekee kwa mwanaume na ikamtofautisha na wanawake. Vilevile ndevu zinamtofautisha na makafiri ambao hunyoa ndevu zao. Ndevu ni pambo la wanaume, ni nuru katika uso na ni alama inayowatofautisha na wanawake. Kwa hiyo haijuziki kwa mwanaume kuzinyoa au kuzipunguza. Hanyoi wala hapunguzi. Vilevile hanyoi pande za mashavu pamoja na kidevu, kwa sababu ndevu ni jina la nywele zinazoota katika taya zote mbili na kidevu. Mashavu na kidevu ndicho kinachoitwa ndevu: nywele za mashavuni, chini ya shavu na chini ya mdomo wa chini. Hivyo haijuzu kuzipunguza wala kuzinyoa, bali ni lazima kuziheshimu, kuziacha zikue na kuzitunza. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuacha ndevu zikue na kunyoa masharubu. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Jitofautisheni na washirikina. Punguzeni masharubu na ziacheni ndevu.”
Imekuja katika Hadiyth nyingine:
Jitofautisheni na waabudia moto.”
“Pungeni masharubu na acheni ndevu zirefuke.”
Imekuja katika tamko nyingine:
“Zitunzeni ndevu na ziacheni zikamilike.”
Kwa hivyo muislamu anapaswa kuziacha ndevu zake zikue na azirefushe. Ni haramu kwake kuzipunguza au kuzinyoa. Hilo ndilo wajibu juu ya muislamu. Aidha muumini haridhii kufanana na dada yake, msichana wake, shangazi yake au mama yake. Inafaa aziache ndevu zake zikue na azitunze ili abaki na sura ya wanaume na aepukane na kujifananisha na waabudu moto na washirikina ambao hunyoa ndevu na kuacha masharubu marefu. Masharubu hupunguzwa na kukatwa, na ndevu huachwa zikue. Hilo ndilo sahihi na lililoamriwa.
Swali: Wanasema kwamba baadhi ya makafiri siku hizi wanaacha ndevu zao zikue?
Jibu: Iwapo wataziacha zikue sifa zote njema ni stahiki ya Allaah. Huenda Allaah akawaongoza wakaingia katika Uislamu. Iwapo watakubaliana nasi katika jambo la kheri, hilo ni jambo jema. Sisi hatuwafuati katika mambo ya shari. Wakituiga katika kuacha ndevu, wakasilimu na kuingia katika dini ya Allaah, basi hilo ni zuri. Lakini haingii akilini kwamba wao waache ndevu nasi tazinyoe, wao waswali nasi tusiswali, wao watoe zakaah nasi tusitoe, hapana. Iwapo watatuendea kinyume, basi sisi tuko katika dini yetu na wao wako katika dini yao. Allaah amesema:
لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ
”Nyinyi mna dini yenu nami nina dini yangu.”[1]
[1] 109:06
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1043/حدود-اللحية-وحكم-حلقها-وتقصيرها
- Imechapishwa: 26/01/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1043/حدود-اللحية-وحكم-حلقها-وتقصيرها
Imechapishwa: 26/01/2026
https://firqatunnajia.com/tuache-kufuga-ndevu-kwa-sababu-makafiri-wengi-hii-leo-wanafuga-ndevu/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket