Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ
”Toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake.”[1]
Baadhi ya watu hutumia Aayah hii kudai kwamba ni lazima kutolewa zakaah katika kila aina ya mazao, hata yale yenye kukua kwa muda mfupi kama nyanya, saladi, karoti, rukula na mengineyo. Je, jambo hili ni sahihi? Ni kiwango gani kinachotolewa kwa ajili ya dhahabu?
Jibu: Allaah (Ta´ala) amezindua uwajibu wa kutoa haki ya nafaka na kwamba siku ya kuvuna mtu anapopata mazao yake anatakiwa kutumia mali hiyo vizuri na kutoa haki yake katika njia ya Allaah, nje ya zakaah. Zakaah ni ´ibaadah ambayo haipimwi kwa maoni ya watu, bali kwa dalili sahihi. Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwepo zakaah katika mbogamboga. Zakaah imeamrishwa kwa nafaka na matunda yanayopimwa kwa kipimo, yanayoweza kuhifadhiwa na kutumiwa sasa na baadaye. Ama matunda yanayoharibika haraka na ambayo hayahifadhiwi wala kupimika kama tikiti na mengi katika matunda, haya hayana zakaah. Isipokuwa zabibu, kwani humo kuna zakaah ya tunda endapo zitafikia kile kiwango kinachotakiwa kutolewa zakaah ya vibaba vitano.
[1] 06:141
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1057/حكم-زكاة-الخضروات-والفواكه
- Imechapishwa: 26/01/2026
Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ
”Toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake.”[1]
Baadhi ya watu hutumia Aayah hii kudai kwamba ni lazima kutolewa zakaah katika kila aina ya mazao, hata yale yenye kukua kwa muda mfupi kama nyanya, saladi, karoti, rukula na mengineyo. Je, jambo hili ni sahihi? Ni kiwango gani kinachotolewa kwa ajili ya dhahabu?
Jibu: Allaah (Ta´ala) amezindua uwajibu wa kutoa haki ya nafaka na kwamba siku ya kuvuna mtu anapopata mazao yake anatakiwa kutumia mali hiyo vizuri na kutoa haki yake katika njia ya Allaah, nje ya zakaah. Zakaah ni ´ibaadah ambayo haipimwi kwa maoni ya watu, bali kwa dalili sahihi. Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwepo zakaah katika mbogamboga. Zakaah imeamrishwa kwa nafaka na matunda yanayopimwa kwa kipimo, yanayoweza kuhifadhiwa na kutumiwa sasa na baadaye. Ama matunda yanayoharibika haraka na ambayo hayahifadhiwi wala kupimika kama tikiti na mengi katika matunda, haya hayana zakaah. Isipokuwa zabibu, kwani humo kuna zakaah ya tunda endapo zitafikia kile kiwango kinachotakiwa kutolewa zakaah ya vibaba vitano.
[1] 06:141
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1057/حكم-زكاة-الخضروات-والفواكه
Imechapishwa: 26/01/2026
https://firqatunnajia.com/nyanya-saladi-karoti-na-rukula-vinatolewa-zakaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket