Swali: Siku hizi twasikia sana kwamba mke si lazima kumhudumia mume wake kama vile kupika na kufua nguo. Tunaomba kutoka kwako ufafanuzi kuhusiana na suala hili.

Jibu: Mwanamke leo kaendelea na wala hamhudumii mume wake. Leo wakati una haja ashughulikie moja katika haja zako, hayupo nyumbani. Mume anakuja na kukaa nyumbani na kusubiri, mke haji ila mpaka ifike mwisho wa usiku. Wanawake wa leo wamekuwa waasi. Ni katika Sunnah wanawake kumhudumia mume wake. Maswahabah wa kike (Radhiya Allaahu ´anhunna) walikuwa wakiwahudumia waume zao; walikuwa wakipika, wakiangalia mambo ya nyumbani. Isitoshe ni Maswahabah wa kike, wanawake bora katika Ummah.

Fatmah bint Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa akibeba maji kwenye mgongo wake mpaka kamba ikaacha alama kwenye mgongo wake. Alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ampe mtumishi akakataa, akakataa kumpa mtumishi. Akamuamrisha atafute msaada kwa Dhikr na Istighfaar, naye ni binti wa Muhammad (´alayhis-Salaam).

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/J49hX6Z6HrI
  • Imechapishwa: 22/09/2020