Swali: Vipi kuhusu anayetofautisha kati ya kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumtukana Mola (Subhaanahu wa Ta´ala)?
Jibu: Sijui tofauti yoyote. Yote mawili ni kuritadi na ni mambo mabaya.
Swali: Kuhusu kukubaliwa kwa tawbah, yule anayemtukana Allaah tawbah yake inakubaliwa na anayemtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haikubaliwi?
Jibu: Baadhi yao wanatofautisha kwa sababu kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni haki ya mwanaadamu, tofauti na kumtukana Allaah kwani ni haki ya Allaah na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) husamehe na hufuta. Huo ndio upande wa utofautishaji. Shaykh Taqiyy-u-d-Diyn (Rahimahu Allaah) ameeleza kwa upana mazungumzo haya katika kitabu cha “as-Swaarim al-Masluul”.
Swali: Je, kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si kumtukana Allaah pia?
Jibu: Hapana, kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani yake kuna maana ya kukanusha. Lililo karibu zaidi – na Allaah anajua zaidi – ni kwamba mwenye kuja akiwa ametubia na mwenye kujutia, basi himdi zote njema anastahiki Allaah, kwani shirki ndio tusi kubwa zaidi. Kumshirikisha Allaah na kumuabudu mwingine ni aina kubwa zaidi ya tusi. Tunamuomba Allaah atulinde.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31509/ما-حكم-من-سب-الرب-او-الرسول-وهل-له-توبة
- Imechapishwa: 30/10/2025
Swali: Vipi kuhusu anayetofautisha kati ya kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumtukana Mola (Subhaanahu wa Ta´ala)?
Jibu: Sijui tofauti yoyote. Yote mawili ni kuritadi na ni mambo mabaya.
Swali: Kuhusu kukubaliwa kwa tawbah, yule anayemtukana Allaah tawbah yake inakubaliwa na anayemtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haikubaliwi?
Jibu: Baadhi yao wanatofautisha kwa sababu kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni haki ya mwanaadamu, tofauti na kumtukana Allaah kwani ni haki ya Allaah na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) husamehe na hufuta. Huo ndio upande wa utofautishaji. Shaykh Taqiyy-u-d-Diyn (Rahimahu Allaah) ameeleza kwa upana mazungumzo haya katika kitabu cha “as-Swaarim al-Masluul”.
Swali: Je, kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si kumtukana Allaah pia?
Jibu: Hapana, kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani yake kuna maana ya kukanusha. Lililo karibu zaidi – na Allaah anajua zaidi – ni kwamba mwenye kuja akiwa ametubia na mwenye kujutia, basi himdi zote njema anastahiki Allaah, kwani shirki ndio tusi kubwa zaidi. Kumshirikisha Allaah na kumuabudu mwingine ni aina kubwa zaidi ya tusi. Tunamuomba Allaah atulinde.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31509/ما-حكم-من-سب-الرب-او-الرسول-وهل-له-توبة
Imechapishwa: 30/10/2025
https://firqatunnajia.com/tofauti-ya-tawbah-ya-anayemtukana-allaah-na-mtume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket