Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ

“Ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah.” (02:04)

Uhakika wa imani ni usadikishaji kamilifu kwa yale waliyoeleza Mitume ambayo ndani yake kuna kunyenyekea kwa viungo. Shani ya imani sio kwa mambo yanayoshuhudiwa kwa kuhisia, kwani mambo kama hayo hapambanuki muislamu kutokamana na kafiri. Shani katika imani ni kwa yale mambo ya ghaibu ambayo hatujayaona wala kuyashuhudia. Tunayaamini kwa sababu yameelezwa na Allaah na Mtume Wake. Hii ndio imani inayompambanua muislamu kutokamana na kafiri. Kwa sababu inahusiana na masadikisho kwa mujibu wa aliyosema Allaah na Mtume Wake.

Muumini anaanini yale yote aliyoeleza Allaah au Mtume Wake. Ni mamoja ameyaona mambo hayo au hakuyaona. Ni mamoja ameyafahamu na kuyaelewa au hayakuingia akilini mwake wala kwenye fahamu zake. Hali hiyo ni tofauti na mazanadiki ambao wanayakadhibisha mambo ya ghaibu. Kwa sababu akili zao pungufu hazikuongozwa kwayo. Matokeo yake wanayakadhibisha yale ambayo hayakuzungukwa na elimu yao. Matokeo yake akili zao zikaharibika na zikatakasika akili za waumini wasadikisha wenye kuongozwa na mwongozo wa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, sid. 29-30
  • Imechapishwa: 03/05/2020