Swali: Mwenye kufa kwa sababu ya kuvuta sigara, yachukuliwa ni kama kujiua?

Jibu: Je, wafikiri kuwa yule anaevuta siraga anavuta kwa sababu afe? Ndio au hapana?

Muulizaji: Hapana!

Jibu: Hivyo basi hachukuliwi kujiua. Lakini yule mwenye kuvaa mabomu tumboni na kwenda na kujilipua kati ya maadui, kaiua nafsi yake mwenyewe. Kuna tofauti baina ya mwenye kukusudia kuiua nafsi yake na baina ya yule ambaye hakukusudia. Lakini kule madhara ya sigara kunapelekea katika kifo, ni dalili yenye nguvu kuwa sigara ni haramu. Na bila shaka sigara ni haramu kutokana na madhara ilio nayo ya kimwili, kitabia na kimali. Hujui kuwa mvuta sigara anaweza kuuza heshima yake kwa ajili ya sigara moja? Kwa vyovyote sigara twaona kuwa ni haramu. Lakini sisemi kuwa mwenye kuvuta kaiua nafsi yake, kwa kuwa hakukusudia kuia nafsi yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (198 B) Tarehe: 1419-11-09/1999-02-24
  • Imechapishwa: 09/04/2022