Kichinjwa cha Hadiy sio kichinjwa cha Udhhiyah. Ni vichinjwa viwili tofauti. Kichinjwa cha Hadiy kinakuwa kwa ajili ya hajj ya Tamattu´. Kichinjwa cha Udhhiyah kinapendeza kwa watu wote hata kama mtu hakuhiji. Udhhiyah ni kichinjwa kinapendeza kwa watu wote; kwa wakazi, watu wa mashambani, vijijini na miji mikubwa. Udhhiyah inakuwa kwa ajili ya mtu mwenyewe na watu wa nyumbani kwake.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja kondoo wawili; mmoja kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wa familia yake na mwingine kwa ajili ya wale wapwekeshaji katika ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kila mwaka alikuwa akichinja kondoo wawili walionona na wenye pembe mbili; mmoja kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wa familia yake na mwingine kwa ajili ya wale wapwekeshaji katika ummah wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hiyo Sunnah, ee mja wa Allaah, ni wewe kuchinja kichinjwa kimoja kwa ajili yako na watu wa nyumbani kwako akiwemo mke wako, familia yako na watoto wako. Hapana vibaya pia ukichinja wanyama wawili au watatu. Usiache kuchinja kama ni muweza. Lakini ukiwa sio muweza:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Lakini ni Sunnah na sio wajibu ikiwa mtu anaweza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/19887/هل-تجزى-الاضحية-عن-هدي-الحج
  • Imechapishwa: 19/07/2024