Tofauti ya dufu na matari/ngoma yasiyofaa kupigwa harusini

Swali: Kuna baadhi ya vitongoji vimenukuu kutoka kwako ya kwamba wewe unajuzisha kwa wanaume kupiga matari katika harusi. Je, ni kweli? Ni ipi hukumu ya wanaume kupiga matari harusini? Tunaomba ubainishe hilo kwa sababu mkutano huu unaenezwa kupitia njia za kaseti.

Jibu: Kuhusu matari hayajuzu si kwa wanaume wala kwa wanawake. Kinachojuzu kwa wanawake ni dufu. Tofauti kati ya dufu na matari ni kuwa dugu unapiga kwa upande mmoja. Ama matari unapiga kwa mbili. Matari yaliyo na pande mbili yanakuwa ni yenye kutoa sauti na mdundiko zaidi kuliko yale yaliyo na upande mmoja. Kwa ajili hiyo imepokelewa katika Sunnah kufaa kwa dufu na hakukupokelewa kitu kuhusu matari. Kuhusu wanaume hatutoi fatwa kujuzu japokuwa kuna wanachuoni wenye kuonelea kuwa inafaa. Lakini sisi hatuonelei kuwa inafaa kwa sababu tunachelea mambo yakapanuka na hatimaye kukatokea madhara kwa wanaume na kwa wanawake.

Yaliyonukuliwa kutoka kwangu kwamba sisi tunawajuzishia wanaume si kweli. Lakini huenda ni kwa vile amesikia nikisema kwamba baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa inafaa ndipo akadhani kuwa mimi nakubaliana nalo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/848