Tofauti kati ya shirki ndogo na njia za shirki

Swali: Ni ipi tofauti kati ya shirki ndogo na njia za shirki?

Jibu: Njia za shirki ni nyingi kama vile kuyajengea makaburi, kujenga misikiti makaburini au kuomba kwa jaha ya fulani. Hizi ni njia zinazopelekea katika kuvuka mipaka. Kuhusu shirki ndogo ni mtu azungumze kwa ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameliita kuwa ni shirki, hata hivyo haifikii katika kiwango cha shirki kubwa. Kama vile kujionesha aina ndogo, lau kama si Allaah na fulani au kuapa kwa asiyekuwa Allaah. Hizi ni miongoni mwa aina ya shirki ndogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24506/ما-الفرق-بين-الشرك-الاصغر-ووساىل-الشرك
  • Imechapishwa: 19/10/2024