Je, anapata dhambi anayefanya njia za shirki?

Swali: Je, anapata dhambi anayefanya njia za shirki?

Jibu: Shirki ndogo ni njia moja wapo inayopelekea katika shirki pia.

Swali: Njia ulizotaja[1] anapata dhambi mwenye kuzifanya kama mfano wa mwenye kuyajengea makaburi?

Jibu: Njia za shirki ni khatari zaidi kuliko aina ya dhambi, kwa sababu njia za shirki zinamwingiza mtu ndani ya shirki. Isitoshe ni Bid´ah. Bid´ah ni mbaya zaidi kuliko maasi. Kuyajengea makaburi na kujenga misikiti juu ya makaburi ni khatari zaidi kuliko aina ya maasi, kwa sababu ni njia inayopelekea katika shirki.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/tofauti-kati-ya-shirki-ndogo-na-njia-za-shirki/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24507/هل-ياثم-الانسان-بفعل-وساىل-الشرك
  • Imechapishwa: 19/10/2024