Tofauti kati ya Karaahat-ut-Tanziyh na Karaahat-ut-Tahriym

Swali: Ni ipi tofauti kati ya machukizo ya utakaso (Karaahat-ut-Tanziyh) na machukizo ya uharamisho (Karaahat-ut-Tahriym)? Vipi nitaweza kutofautisha kati ya haya mawili?

Jibu: Machukizo ya utakaso hakuna madhambi ndani yake. Anapewa thawabu yule mwenye kuacha na haadhibiwi yule mwenye kuyafanya. Haya ndio machukizo ya utakaso. Ama machukizo ya uharamisho, anapata dhambi mwenye kuyafanya na anapawe thawabu mwenye kuyaacha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-5-25.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014