Swali: Ni upi msingi wa Da´wah ya Salafiyyah? Na ina maingiliano yapi na Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab? Na je makundi ya leo katika Jamaa´at-ut-Tabliygh na al-Ikhwaan al-Muslimuun ni katika matunda ya Daw´ah ya Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab?

Jibu: Da´wah ni Da´wah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanaojikosoa baada yake katika watengenezaji. Ni Da´wah ya Tawhiyd na kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall) peke Yake na kutubia kwa madhambi na maasi. Hii ndo Da´wah sahihi.

Ama Da´wah zingine zisizojali Tawhiyd wala ´Aqiydah. Hizi ni Da´wah ambazo si sahihi. Da´wah kama hizi zina maslahi yake na makusudio yake. Kwa kuwa kama kweli wanalingania kwa ajili ya Allaah, basi wangelianza kwa ´Aqiydah kama walivyofanya Mitume (´alayhimus-Salaam). Kitu cha kwanza walichoanza nacho kwa Ummah zao ni kuwalingania watu katika ´Aqiydah na kuzitengeneza ´Aqiydah. Huu ndo mfumo wa kweli na sahihi. Na mwenye kwenda kinyume nao, hakika halinganii kwa Allaah. Bali analingania kwa maslahi yake ayatakayo yeye.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=128762
  • Imechapishwa: 03/09/2020