Thawabu za mwanafunzi na madhambi yanayofutwa

Elimu inachangia kusamehewa madhambi na kuongeza thawabu. Mwanafunzi anapojifunza thawabu zake zinaongezeka:

إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ

“Hakika mema yanaondosha maovu.” (11:114)

Kama tulivyosema kusoma ni katika ´ibaadah kubwa, fadhila na thawabu. Ina maana kwamba kusoma ni katika matendo bora kabisa yanayoyaondosha madhambi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ

“Simamisha swalah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku, hakika mema yanaondosha maovu. Hivyo ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mche Allaah popote ulipo. Fuatisha tendo jema baada ya tendo baya italifuta. Tangamana na watu kwa tabia njema.”

Yanathibitisha kuwa mwanafunzi thawabu zake zinaongezeka ambayo yanafuta madhambi yake. Anaposoma, anapoandika, anapohudhuria darsa au anapokariri na kuhifadhi kwa njia njema, analipwa thawabu. Kadhalika matendo yake mema yanafuta matendo yake maovu midhali ni mwenye kujiepusha na yale madhambi makubwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Fadhwl-ul-´Ilm wa Ahlihi wa Swifatuhum
  • Imechapishwa: 12/03/2017