Swali: Umegusia kuhusu kukata swawm kwa tende kavu. Je, Sunnah ni mtu kula tende tatu na zaidi au inatosha kula tende moja kisha mtu baada ya hapo anywe kahawa na mfano wa hivo kwa yule anayekata swawm kwa tende saba. Ni lazima ale tende moja halafu anywe baada ya kula tende saba?

Jibu: Kwa hali yoyote mtu anatakiwa kukata swawm kwa tende. Uchache wake ni tatu. Lakini baadhi ya watu katika majira ya joto wanakuwa na kiu na mdomo unakuwa mkavu. Hivyo inapelekea wanahitajia kunywa maji pia. Hakuna neno. Jambo hili ni pana. Lakini ukiweza kula tende tatu kabla ya kuanza kunywa ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1374
  • Imechapishwa: 29/11/2019