Tawbah ya mfanya liwati inakubaliwa?

Swali 182: Ana tawbah mwenye kufanya jarima ya liwati?

 Jibu: Tawbah ni yenye kukubalika. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ

”Hakika Mimi ni Mwingi mno wa kusamehe kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema kisha akaendelea kuongoka.”[1]

Yaliyopokelewa kwamba iwapo mlawiti ataoga kwa maji ya bahari hatotwaharika ni Hadiyth ya uongo ambayo haikusihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah ndiye anajua zaidi.

[1] 20:82

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 364
  • Imechapishwa: 05/10/2019