Tasmiyah wakati wa kuchinja wanyama wengi

Swali: Wakati ninapochinja kondoo mia mfano. Je, inatosha kutaja jina moja au hapana?

Jibu: Kila kondoo unahitaji kumtajia jina la Allaah. Ikiwa kuna mashine inayowachinja kwa haraka, basi ataje juu ya wote. Tunatumaini kwamba inatosha – Allaah akitaka. Lakini ikiwa anawachinja kwa mkono wake wa kulia, ataje. Ikiwa ni kwa mashine inayopita katika koo zao kwa haraka na akataja juu ya mashine hiyo kwa haraka, tunatumaini kwamba hilo linatosha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1093/ذبح-مجموعة-من-الغنم-بتسمية-واحدة
  • Imechapishwa: 15/12/2025