Swali: Je, inajuzu suala la kuachika likawa mikononi mwa mwanamke iwapo atashurutisha hivyo na mwanaume akakubali? Naomba dalili pia?

Jibu: Mwanzoni mwa ndoa, hapana. Talaka ipo mikononi mwa wanaume:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake.”[1]

Lakini baada ya ndoa, ikiwa ataifanya talaka iwe imefungamanishwa na kitendo chake au kutaka kwake, basi hapana vibaya. Dalili ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Waislamu wapo juu ya masharti yao.”

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakika masharti yenye haki zaidi ya kutekelezwa ni yale mliyoyafanya halali tupu zenu kwa ajili yake.”

Lakini asili ya talaka ipo mikononi mwa mume. Ikiwa atamuwakilisha mke wake ajitaliki mwenyewe au akaifungamanisha talaka na kitendo chake fulani, mfano kwa kusema ”ukitoka au ukiongea na fulani”, basi itakuwa yenye kupita muda wa kuwa amekusudia talaka.

[1] 04:34

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30967/هل-يجوز-ان-تكون-العصمة-في-يد-المراة
  • Imechapishwa: 18/09/2025