Amemjamii mkewe baada ya kutoka Ihraam ya kwanza kwa kusahau

Swali: Kuna mtu aliyekuwa katika Hajj amemjamii mke wake baada ya kutoka Ihraam ya kwanza hali ya kusahau. Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Ikiwa alikuwa amesahau, sahihi ni kwamba hakuna kitu kinachomlazimu:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Allaah akasema:

”Nimefanya hivo.”

Hivyo ikiwa kweli alikuwa amesahau na ni mkweli, basi hakuna chochote kinachomlazimu. Namna hii ndio sahihi.

[1] 14-15

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30956/حكم-من-جامع-زوجته-بعد-التحلل-الاول-ناسيا
  • Imechapishwa: 18/09/2025