Swali: Mwenye kupinga kitu ambacho kinajulikana fika katika dini kujuzu kwake. Je, yeyote anaweza kumkufurisha au hili ni jambo maalum kwa wanachuoni?

Jibu: Ikiwa ni mjinga na hajui mambo ya dini inatakiwa kumbainishia na kuwekewa wazi. Akiendelea kufanya hivo baada ya kujua na ubainifu, anahukumiwa kuritadi. Lakini wenye kufanya hivi ni wanachuoni waliobobea katika elimu. Si haki ya kila mmoja kukufurisha na kuhukumu kuritadi. Si haki ya watu wote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (37) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-1-25.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020