Takbiyr baada ya zile swalah tano za faradhi misikitini

´Iyd-ul-Adhwhaa inaizidi ´Iyd-ul-Fitwr kwa usuniwaji wa Takbiyr ndani yake. Nazo ni zile Takbiyr zilizowekwa katika Shari´ah baada ya kila swalah ya faradhi katika mkusanyiko. Imamu anatakiwa kuwageukia waswaliji kisha alete Takbiyr na wao pia walete Takbiyr. ad-Daaraqutwniy na Ibn Abiy Shaybah wamepokea kupitia kwa Jaabir ambaye amesimulia:

“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposwali Fajr katika siku ya kufuata ya ´Arafah anasema:

“Allaahu Akbar… “

Takbiyr zilizofungamanishwa baada ya kila swalah kwa ambaye hayuko katika Ihraam zinaanza kuanzia swalah ya Fajr siku ya ´Arafah mpaka swalah ya ´Aswr ile siku ya mwisho ya kuchinja. Kwa ambaye yuko katika Ihraam Takbiyr zilizofungamanishwa kwake zinaanza kuanzia swalah ya Dhuhr ile siku ya kwanza ya kuchinja mpaka ´Aswr ile siku ya mwisho ya kuchinja. Kwa sababu kabla ya hapo yeye ameshughulishwa na kuleta Talbiyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mulakhaswsw-ul-Fiqh (01/279)
  • Imechapishwa: 30/07/2020