Swali: Je, inafaa kuwatukana Ahl-ul-Bid´ah na kuwaeleza kwa njia inayopelekea matusi wakati wa kutahadharisha nao?

Jibu: Hakuna haja ya kulaani. Hili halitatui tatizo. Hata hivo yanatakiwa kubainishwa makosa walionayo. Ubainifu na matahadharisho juu ya Bid´ah zao inatakiwa iwe kwa njia ya kielimu ili watu wasitumbukie katika Bid´ah zao na hivyo wakaangamia. Asiwatukane na wala asiwashutumu. Bali abainishe makosa yao na kwenda kwao kinyume.

Bid´ah zinatofautiana. Kuna Bid´ah kubwa ambazo mwenye nazo anatukanywa na kutahadharishwa. Bid´ah nyenginezo hazifikii kiwango hicho. Hata hivyo kosa la mzushi huyo linatakiwa kubainishwa. Na ikiwa ni miongoni mwa wanaozilingania, basi anapaswa kutahadharishwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=4i3YojbP2rk
  • Imechapishwa: 17/02/2024