Swali: Ni ipi hukumu ya makosa ya baadhi ya watawala au wanachuoni yanayoenezwa kwenye intaneti ambayo hayazidishi chochote katika kuitengeneza jamii ya Kiislamu isipokuwa maovu zaidi na kuleta tofauti na khaswa leo?

Jibu: Mnajua kuwa walinganizi wa fitina na wa upotevu lengo leo ni kutaka kufarikisha waislamu na kubatilisha hukumu ya Kiislamu na badala yake demokrasia, uanasekula na huria ndio ichukue nafasi. Hili ndilo wanalolitaka. Wametumia njia hizi za mawasiliano ili kueneza fikira na utata wao. Tahadhari nao na tahadharisheni nao kweli kweli na bainisheni kuwa ni walinganizi wa fitina, wanaeneza mashaka na hoja tata na kuwachochea watu katika mapinduzi na uasi kwa mtawala.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–14330720.mp3
  • Imechapishwa: 08/06/2020