Swali: Nilioa na kumpa mke wangu tafsiri ya Qur-aan ya Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) kama mahari. Baadaye mwanafunzi mmoja akanambia kuwa mahari hayo hayasihi kwa sababu hayana maana yoyote. Je, maneno yake ni sahihi?
Jibu: Vipi hayana maana yoyote? Tafsiri ya Qur-aan ya Ibn Kathiyr haina maana yoyote? Haya ni maneno ya mjinga, sio maneno ya mwanafunzi.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
- Imechapishwa: 27/07/2023