Wale wenye kufasiri Shahaadah kwa mfumo wa kwamba hakuna muumbaji na mwenye kuruzuku anayenufaisha na kudhuru isipokuwa Allaah wamefanya kosa kubwa. Nayo ni tafsiri ya Jamaa´at-ut-Tabliygh katika hali ya uandishi.

Vile vile tafsiri ya al-Ikhwaan al-Muslimuun ya Shahaadah kwamba hakuna mwenye kuhukumu isipokuwa Allaah ni kosa kubwa. Hawakuifasiri Shahaadah kwa tafsiri ya Salaf, nayo ya kwamba Shahaadah hakuna mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah ina maana kuwa hakuna yeyote anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah.

  • Mhusika: ´Allâmah Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhalî
  • Mfasiri: at-Ta´liyqaat al-Jiyaad ´alaa Kitaab Tatwhiyr-il-I´tiqaad, uk. 76
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 22/04/2015