Swali: Unasemaje kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh na unanishauri kutoka nao?

Jibu: Nakushauri ulinganie kwa Allaah kwa mfumo wa kinabii. Ikiwa uko na elimu na umaizi basi lingania kwa Allaah kwa mfumo wa kinabii.

Kuhusu mapote na makundi yanayoenda kinyume na mfumo wa kinabii tahadhari nayo na wala usitoke nayo. Miongoni mwa mfumo wa kinabii ni kuanza kulingania katika Tawhiyd. Je, Jamaa´at-ut-Tabliygh wanalingania katika Tawhiyd? Hatujawahi kuyasikia haya wala kuyatambua. Bali wanakataza kulingania katika Tawhiyd na wanasema:

“Msitaje Tawhiyd! Mnafarikisha kati ya watu.”

Hivi ndivo wanavosema. Ni kundi lipi hili? Ni ulinganizi upi huu?

Swali. Baadhi ya ndugu wamewekea taaliki jambo hili na kusema Jamaa´at-ut-Tabliygh wanatofautiana kutegemea na ile nchi wametokea.

Jibu: Hapana! Hapana! Hiyo ni Jamaa´at-ut-Tabliygh. Lakini baadhi ya maeneo ni walaini na kwenginepo wanajidhihirisha. Vinginevyo Jamaa´at-ut-Tabliygh ni moja. Kinachozingatiwa ni msingi wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: al-Farq bayn at-Taysiyr ash-Shar´iy wal-Mu´aaswir
  • Imechapishwa: 21/05/2022