Swali: Unasemaje juu ya wale wanaokataza kutahadharisha Jamaa´at-ut-Tabliygh na wanasema kuwa wamewanufaisha watu wengi?

Jibu: Usawa ni kuwatahadharisha. Sisi hatuna shaka juu ya dini yetu. Sisi tuko na Da´wah; Da´wah ya Tawhiyd ambayo iliasisiwa na Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na wakapita juu yake watu wa nchi. Ni Da´wah sahihi. Hatuhitajii kufuata makundi yanayotoka huku na kule na kusema kuwa wamenufaisha. Ulinganizi wa Tawhiyd ni wenye manufaa zaidi na zaidi na ni bora.

Kundi hili halijulikani. Kumetajwa juu yake mambo mengi. Kumetungwa vitabu vinavyotahadharisha nalo. Vimeandikwa na watu waliosafiri huko na wakaona kwa macho yao ya kwamba kundi hili limezuliwa. Kwa hivyo haijuzu kutendea kazi mfumo wake na kulifata.

Kuna haja gani ya kufanya hivo? Sisi tuko na mfumo sahihi, salama na ulio wazi ambao unatendewa kazi na wakazi wa nchi hii. Wamepita juu ya njia hii salama mpaka sasa karibu miaka 200. Mnataka kufanya nini na mirengo mingine na mifumo mingine ilihali hatujui iko na nini na ni nani ambaye yuko nyuma yake?

Manufaa hayaangaliwi kwa kiwango. Watu wanapenda Bid´ah zaidi kuliko wanavoipenda  Sunnah. Mtu akiwalingania katika Sunnah, basi wote wanahisi uzito isipokuwa wachache mno. Mtu akiwalingania katika Bid´ah, basi wanafanya haraka na kupata uchangamfu. Kwa sababu shaytwaan ndiye anawatia nguvu katika hilo. Kwa hivyo kinachoangaliwa sio wingi wa wafuasi na manufaa yao. Manufaa yako wapi kwao? Je, wao wanajua Tawhiyd? Waulizeni maana ya “Laa ilaaha illa Allaah” na sharti zake na nguzo zake na ni vipi vichenguzi vyake. Hawajui chochote. Hawajui chochote kuhusu Tawhiyd. Hiki ni kitu kimeonekana na kinatambulika kwao. Wengi wao ni watu wa kawaida, sio wanafunzi. Hawajui chochote. Ni vipi watakuwa walinganizi ilihali ni watu wa kawaida na wajinga?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Waajib-ul-Muslim tijaah al-Afkaar wal-Aaraa’ al-Mudhwillah Tarehe: 1428-10-29/2007-11-09
  • Imechapishwa: 21/05/2022