Swali: Je, inashurutishwa kulala na nia usiku kwa ajili ya kufunga siku sita za Shawwaal? Ikiwa mtu ataamka asubuhi katika moja ya siku za Shawwaal na bado hajala chochote – je, atahesabiwa siku hiyo?

Jibu: Swawm ya kujitolea haishurutishwi kulaza nia usiku. Hakuna vibaya ikiwa mtu ataanza kufunga katikati ya mchana, lakini funga yake itakuwa na upungufu. Na ikiwa atafunga kuanzia mwanzoni mwa mchana, basi hiyo ni bora na kamili zaidi. Lakini ikiwa amefunga kuanzia katikati ya mchana, basi swawm yake inakuwa pungufu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25438/هل-يشترط-تبييت-النية-لصيام-الست-من-شوال
  • Imechapishwa: 20/03/2025