Swali: Ni ipi hukumu ya kufunga jumatatu na alkhamisi? Ni ipi katika siku mbil hizo iliyokokotezwa zaidi?

Jibu: Inapendeza kufunga siku ya jumatatu na alkhamisi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Matendo yanaonyeshwa kwa Allaah jumatatu na alkhamisi. Hivyo napenda yaonyeshwe matendo yangu hali ya kuwa nimefunga.”[1]

Kufunga jumatatu ndio muhimu zaidi kuliko alkhamisi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu kufunga siku ya jumatatu, akasema:

“Hiyo ni siku ambayo nimezaliwa, nikatumilizwa na kuteremshiwa wahy.”[2]

[1] at-Tirmidhiy (747). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (747).

[2] Muslim (1162).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/15-16)
  • Imechapishwa: 04/08/2026